1Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake,
2Yeye ambaye njia zake ni nyofu humcha Bwana,
3Mazungumzo ya mpumbavu huleta fimbo mgongoni mwake,
4Pale ambapo hakuna mafahali, hori ni tupu,
5Shahidi mwaminifu hadanganyi,
6Mwenye mzaha huitafuta hekima na haipati,
7Kaa mbali na mtu mpumbavu,
8Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake,
9Wapumbavu hudhihaki kujirekebisha kutoka dhambi,
10Kila moyo hujua uchungu wake wenyewe,
11Nyumba ya mwovu itaangamizwa,
12Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu,
13Hata katika kicheko moyo waweza kuuma,
14Wasio na imani watapatilizwa kikamilifu kwa ajili ya njia zao,
15Mtu mjinga huamini kila kitu,
16Mtu mwenye hekima humcha Bwana na kuepuka mabaya,
17Mtu anayekasirika kwa haraka hufanya mambo ya upumbavu,
18Mjinga hurithi upumbavu,
19Watu wabaya watasujudu mbele ya watu wema,
20Maskini huepukwa hata na majirani zao,
21Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi,
22Je, wale wanaopanga ubaya hawapotoki?
23Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida,
24Utajiri wa wenye hekima ni taji yao,
25Shahidi wa kweli huokoa maisha,
26Yeye amchaye Bwana ana ngome salama,
27Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima,
28Wingi wa watu ni utukufu wa mfalme,
29Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi,
30Moyo wenye amani huupa mwili uzima,
31Yeye amwoneaye maskini huonyesha dharau kwa Muumba wao,
32Waovu huangamizwa kwa matendo yao maovu,
33Hekima hukaa katika moyo wa mwenye ufahamu
34Haki huinua taifa,
35Mfalme hupendezwa na mtumishi mwenye hekima,