1Kisha Ayubu akajibu:
2“Laiti uchungu wangu ungeweza kupimwa,
3Kwa kuwa hakika ingekuwa nzito kuliko mchanga wa bahari zote,
4Mishale ya Mwenyezi iko ndani yangu,
5Je, punda-mwitu hulia akiwa na majani,
6Je, chakula kisicho na ladha huliwa bila chumvi,
7Ninakataa kuvigusa;
8“Laiti ningepata haja yangu,
9kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda,
10Ndipo bado ningekuwa na hii faraja,
11“Ninazo nguvu gani, hata niendelee kutumaini?
12Je, mimi nina nguvu za jiwe?
13Je, ninao uwezo wowote wa kujisaidia mimi mwenyewe,
14“Mtu anayekata tamaa angetazamia moyo wa kujitoa wa rafiki zake,
15Lakini ndugu zangu sio wa kutegemewa,
16wakati vimefunikwa barafu iyeyukayo,
17lakini hukauka majira ya ukame,
18Misafara hugeuka kutoka njia zake;
19Misafara ya Tema inatafuta maji,
20Wamedhikika, kwa sababu walikuwa na matumaini;
21Sasa nanyi mmethibitika kwamba hamna msaada wowote;
22Je, nimewahi kusema, ‘Toeni kitu kwa ajili yangu,
23au niokoeni mikononi mwa adui,
24“Nifundisheni, nami nitanyamaza kimya;
25Tazama yalivyo ya kuumiza maneno ya kweli!
26Je, mna maana ya kuyasahihisha ninayosema,
27Mngeweza hata kupiga kura kwa ajili ya yatima,
28“Lakini sasa kuweni na huruma mkaniangalie mimi.
29Tulizeni hasira, msiwe wadhalimu;
30Je, pana uovu wowote midomoni mwangu?