1Ndipo Ayubu akajibu:
2“Je, mtaendelea kunitesa mpaka lini,
3Mara kumi hizi mmenishutumu;
4Kama ni kweli nimepotoka,
5Kama kweli mngejitukuza wenyewe juu yangu,
6basi jueni kuwa Mungu amenitendea yaliyo mabaya,
7“Ingawa ninalia, ‘Nimetendewa mabaya!’ sipati jibu;
8Yeye ameizuia njia yangu hivyo siwezi kupita;
9Amenivua heshima yangu,
10Amenibomoa kila upande hadi nimeisha;
11Hasira yake imewaka juu yangu;
12Majeshi yake yananisogelea kwa nguvu;
13“Amewatenga ndugu zangu mbali nami;
14Watu wa jamaa yangu wamekwenda mbali;
15Wageni wangu na watumishi wangu wa kike wananiona kama mgeni;
16Namwita mtumishi wangu, wala haitiki,
17Pumzi ya kinywa changu ni kinyaa kwa mke wangu;
18Hata watoto wadogo hunidhihaki;
19Rafiki zangu wa moyoni wote wananichukia kabisa;
20Mimi nimebaki mifupa na ngozi tu;
21“Nihurumieni, rafiki zangu, kuweni na huruma,
22Kwa nini mnanifuatia kama Mungu afanyavyo?
23“Laiti maneno yangu yangewekwa kwenye kumbukumbu,
24kwamba yangechorwa kwenye risasi kwa kifaa cha chuma,
25Ninajua kwamba Mkombozi19:25 Au: Mtetezi. wangu yu hai,
26Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa,
27mimi nitamwona kwa macho yangu mwenyewe:
28“Kama mkisema, ‘Tazama tutakavyomwinda,
29ninyi wenyewe uogopeni upanga,