1“Nayachukia sana haya maisha yangu;
2Nitamwambia Mungu: Usinihukumu,
3Je, inakupendeza wewe kunionea,
4Je, wewe una macho ya kimwili?
5Je, siku zako ni kama zile za mwanadamu,
6ili kwamba utafute makosa yangu
7ingawa wajua kuwa mimi sina hatia,
8“Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunifanya.
9Kumbuka kuwa ulinifinyanga kama udongo wa mfinyanzi.
10Je, wewe hukunimimina mimi kama maziwa,
11ukanivika ngozi na nyama,
12Umenipa uhai na kunitendea wema,
13“Lakini hili ndilo ulilolificha moyoni mwako,
14Kama nilifanya dhambi, ungekuwa umeniona,
15Kama nina hatia, ole wangu!
16Kama nikiinua kichwa changu juu, unaninyatia kama simba,
17Wewe waleta mashahidi wapya dhidi yangu
18“Kwa nini basi ulinitoa tumboni?
19Laiti nisingekuwako kamwe,
20Je, siku zangu chache si zimekaribia kuisha?
21kabla sijaenda mahali ambapo hakuna kurudi tena,
22nchi ya giza kuu sana,