1Mshukuruni Bwana, kwa kuwa yeye ni mwema,
2Waliokombolewa wa Bwana na waseme hivi,
3wale aliowakusanya kutoka nchi mbalimbali,
4Baadhi yao walitangatanga jangwani,
5Walikuwa na njaa na kiu,
6Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao,
7Akawaongoza kwa njia iliyo sawa
8Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,
9kwa maana yeye humtosheleza mwenye kiu,
10Wengine walikaa gizani na katika huzuni kuu,
11kwa sababu walikuwa wameasi
12Aliwatumikisha kwa kazi ngumu;
13Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao,
14Akawatoa katika giza na huzuni kuu
15Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,
16kwa kuwa yeye huvunja malango ya shaba
17Wengine wakawa wapumbavu kutokana na uasi wao,
18Wakachukia kabisa vyakula vyote,
19Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao,
20Akalituma neno lake na kuwaponya,
21Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,
22Na watoe dhabihu za kushukuru,
23Wengine walisafiri baharini kwa meli,
24Waliziona kazi za Bwana,
25Kwa maana alisema na kuamsha tufani
26Yakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini,
27Walipepesuka na kuyumbayumba kama walevi,
28Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao,
29Akatuliza dhoruba kwa mnongʼono,
30Walifurahi ilipokuwa shwari,
31Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,
32Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu,
33Yeye aligeuza mito kuwa jangwa,
34nchi izaayo ikawa ya chumvi isiyofaa,
35Aligeuza jangwa likawa madimbwi ya maji,
36aliwaleta wenye njaa wakaishi humo,
37Walilima mashamba na kupanda mizabibu,
38Mungu aliwabariki, hesabu yao ikaongezeka sana,
39Kisha hesabu yao ilipungua, na walinyenyekeshwa
40Yeye ambaye huwamwagia dharau wakuu,
41Lakini yeye aliwainua wahitaji katika taabu zao,
42Wanyofu wataona na kufurahi,
43Yeyote aliye na hekima, ayasikie mambo haya,