1Mithali za Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli:
2Kwa kupata hekima na nidhamu;
3kwa kujipatia nidhamu na busara,
4huwapa busara wajinga,
5wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao,
6kwa kufahamu mithali na mifano,
7Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa,
8Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,
9Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako,
10Mwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi,
11Kama wakisema, “Twende tufuatane;
12tuwameze wakiwa hai kama kaburi,1:12 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
13Tutapata aina zote za vitu vya thamani
14Njoo ushirikiane nasi,
15Mwanangu, usiandamane nao.
16kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi,
17Tazama ni jinsi gani ilivyo kazi bure kutandaza wavu
18Watu hawa huvizia kumwaga damu yao wenyewe;
19Huu ndio mwisho wa wote ambao wanajipatia mali kwa hila;
20Hekima huita kwa sauti kuu barabarani,
21kwenye makutano ya barabara za mji
22“Enyi wajinga, mtangʼangʼania ujinga wenu hadi lini?
23Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu,
24Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita
25kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote
26mimi nami nitawacheka katika maafa yenu,
27wakati janga litawapata kama tufani,
28“Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu;
29Kwa kuwa walichukia maarifa,
30kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu,
31watakula matunda ya njia zao,
32Kwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua,
33Lakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama,