1“Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke
2Huchanua kama ua kisha hunyauka;
3Je, unamwekea jicho lako mtu kama huyo?
4Ni nani awezaye kutoa kitu safi kutoka kitu najisi?
5Siku za mwanadamu zimewekewa mpaka;
6Hivyo angalia mbali umwache,
7“Kwa maana lipo tumaini kwa mti;
8Mizizi yake yaweza kuchakaa ardhini
9lakini kwa kupata dalili ya maji utachipua
10Lakini mwanadamu hufa, na huo ndio mwisho wake;
11Kama vile maji yatowekavyo katika bahari,
12ndivyo mwanadamu alalavyo chini asiamke;
13“Laiti kama ungenificha kaburini,14:13 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
14Je, kama mtu akifa, aweza kuishi tena?
15Utaniita nami nitakuitika;
16Hakika ndipo utakapozihesabu hatua zangu,
17Makosa yangu yatafungiwa kwa lakiri kwenye mfuko,
18“Lakini kama mlima umomonyokavyo na kufikichika
19kama maji yamalizavyo mawe,
20Humshinda mara moja kwa daima, naye hutoweka;
21Kama wanawe wakipewa heshima, yeye hafahamu;
22Yeye hasikii kingine isipokuwa maumivu ya mwili wake mwenyewe,