1Basi watu hawa watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa kuwa alikuwa mwadilifu machoni pake mwenyewe.
2Lakini Elihu mwana wa Barakeli, wa kabila la Buzi wa jamaa ya Ramu, akamkasirikia sana Ayubu, kwa sababu ya kujihesabia haki mwenyewe badala ya Mungu.
3Pia aliwakasirikia hao rafiki watatu wa Ayubu, kwa sababu hawakuweza kupata njia ya kuthibitisha ya kuwa hayo maneno ya Ayubu hayakuwa ya kweli, nao bado walikuwa wamemlaumu.
4Basi Elihu alikuwa amesubiri kwanza waongee na Ayubu kwa sababu walikuwa na umri mkubwa kumliko yeye.
5Lakini alipoona watu hao watatu hawakuwa na kitu zaidi cha kusema, hasira yake ikaamka.
6Basi Elihu mwana wa Barakeli wa kabila la Buzi akasema:
7Nilifikiri, ‘Yafaa umri useme,
8Lakini ni Roho iliyoko ndani ya mwanadamu,
9Sio wazee peke yao walio na hekima,
10“Kwa hiyo nasema: Nisikilizeni mimi;
11Nilingojea mlipokuwa mnaongea,
12niliwasikiliza kwa makini.
13Msiseme, ‘Tumepata hekima;
14Lakini Ayubu hajayapanga maneno yake dhidi yangu,
15“Wametiwa hofu na hawana la zaidi la kusema;
16Je, ningoje sasa kwa sababu wamekuwa kimya,
17Mimi nami nitakuwa na la kusema;
18Kwa kuwa nimejawa na maneno,
19ndani yangu niko kama chupa iliyojazwa divai,
20Ni lazima niseme ili niweze kutulia;
21Sitampendelea mtu yeyote,
22kwa kuwa kama ningekuwa stadi wa kujipendekeza,