1Ndipo Ayubu akajibu:
2“Hata leo malalamiko yangu ni chungu;
3Laiti ningefahamu mahali pa kumwona;
4Ningeliweka shauri langu mbele zake,
5Ningejua kwamba angenijibu nini,
6Je, angenipinga kwa nguvu nyingi?
7Hapo mtu mwadilifu angeweka shauri lake mbele zake,
8“Lakini nikienda mashariki, hayupo;
9Anapokuwa kazini pande za kaskazini, simwoni;
10Lakini anaijua njia niiendeayo;
11Nyayo zangu zimefuata hatua zake kwa karibu;
12Sijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake;
13“Lakini yeye husimama peke yake; ni nani awezaye kumpinga?
14Hutimiliza maagizo yake dhidi yangu,
15Hiyo ndiyo sababu ninaingiwa na hofu mbele zake;
16Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia;
17Hata hivyo sijanyamazishwa na giza,