We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

Isaya 20

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← Isaya 19 Isaya Isaya 21 →

1Katika mwaka ule ambao jemadari mkuu alitumwa na Mfalme Sargoni wa Ashuru, naye akaja mpaka Ashdodi, akaushambulia na kuuteka,

2wakati ule Bwana alisema kwa kinywa cha Isaya mwana wa Amozi. Akamwambia, “Vua nguo ya gunia kutoka mwilini mwako na viatu kutoka miguuni mwako.” Naye akafanya hivyo, akatembea huku na huko uchi, bila viatu.

3Kisha Bwana akasema, “Kama vile mtumishi wangu Isaya alivyotembea uchi na bila viatu kwa miaka mitatu, kama ishara na dalili mbaya dhidi ya nchi ya Misri na Kushi,

4vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawaongoza mateka wa Wamisri, na watu wa uhamisho wa Kushi, uchi na bila viatu, vijana hata wazee, wakiwa matako wazi, kwa aibu ya Wamisri.

5Wale waliotegemea Kushi na kujivunia Misri wataogopa na kuaibika.

6Katika siku ile watu wanaoishi katika pwani hii watasema, ‘Tazama lililowapata wale tuliowategemea, wale tuliowakimbilia kwa msaada na wokovu kutoka mikononi mwa mfalme wa Ashuru! Tutawezaje basi kupona?’ ”

← Isaya 19 Isaya Isaya 21 →