We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

Mwanzo 10

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← Mwanzo 9 Mwanzo Mwanzo 11 →

1Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.

2Wana wa Yafethi walikuwa:

3Wana wa Gomeri walikuwa:

4Wana wa Yavani walikuwa:

5(Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.)

6Wana wa Hamu walikuwa:

7Wana wa Kushi walikuwa:

8Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani.

9Alikuwa mwindaji hodari mbele za Bwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za Bwana.”

10Vituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari.

11Kutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala,

12na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.

13Misraimu alikuwa baba wa:

14Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.

15Kanaani alikuwa baba wa:

16Wayebusi, Waamori, Wagirgashi,

17Wahivi, Waariki, Wasini,

18Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.

19na mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.

20Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

21Shemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.

22Wana wa Shemu walikuwa:

23Wana wa Aramu walikuwa:

24Arfaksadi alikuwa baba wa Shela,

25Eberi akapata wana wawili:

26Yoktani alikuwa baba wa:

27Hadoramu, Uzali, Dikla,

28Obali, Abimaeli, Sheba,

29Ofiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.

30Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki.

31Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

32Hizi ndizo koo za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.

← Mwanzo 9 Mwanzo Mwanzo 11 →