We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

Kutoka 15

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← Kutoka 14 Kutoka Kutoka 16 →

1Ndipo Mose na Waisraeli wakamwimbia Bwana wimbo huu:

2Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu;

3Bwana ni shujaa wa vita;

4Magari ya vita ya Farao na jeshi lake

5Maji yenye kina yamewafunika,

6“Mkono wako wa kuume, Ee Bwana

7Katika ukuu wa utukufu wako,

8Kwa pumzi ya pua zako

9“Adui alijivuna,

10Lakini ulipuliza kwa pumzi yako,

11“Ni nani miongoni mwa miungu aliye kama wewe, Ee Bwana?

12Uliunyoosha mkono wako wa kuume

13“Katika upendo wako usiokoma utawaongoza

14Mataifa watasikia na kutetemeka,

15Wakuu wa Edomu wataogopa,

16vitisho na hofu vitawaangukia.

17Utawaingiza na kuwapandikiza

18Bwana atatawala

19Farasi wa Farao, magari yake ya vita na wapanda farasi wake walipoingia baharini, Bwana aliyarudisha maji ya bahari yakawafunika, lakini wana wa Israeli walipita baharini mahali pakavu.

20Kisha Miriamu yule nabii mke, ndugu yake Aroni, akachukua matari mkononi mwake na wanawake wote wakamfuata na matari yao wakicheza.

21Miriamu akawaimbia:

22Kisha Mose akawaongoza Israeli kutoka Bahari ya Shamu na kuingia katika Jangwa la Shuri. Kwa siku tatu walisafiri jangwani bila kupata maji.

23Walipofika Mara, hawakuweza kunywa maji yake kwa sababu yalikuwa machungu. (Ndiyo sababu mahali hapo panaitwa Mara15:23 Mara maana yake ni Chungu.)

24Kwa hiyo watu wakamnungʼunikia Mose, wakisema, “Tunywe nini?”

25Ndipo Mose akamlilia Bwana, naye Bwana akamwonyesha kipande cha mti. Akakitupa ndani ya maji, nayo maji yakawa matamu.

26Mungu akasema, “Kama mkisikiliza kwa bidii sauti ya Bwana Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa machoni pake, kama mkiyatii maagizo yake na kuzishika amri zake zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi Bwana, niwaponyaye.”

27Kisha wakafika Elimu, mahali palipokuwa na chemchemi kumi na mbili, na miti sabini ya mitende, wakapiga kambi huko karibu na maji.

← Kutoka 14 Kutoka Kutoka 16 →