We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

Mhubiri 3

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← Mhubiri 2 Mhubiri Mhubiri 4 →

1Kuna wakati kwa ajili ya kila jambo,

2wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa,

3wakati wa kuua na wakati wa kuponya,

4wakati wa kulia na wakati wa kucheka,

5wakati wa kutawanya mawe na wakati wa kukusanya mawe,

6wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza,

7wakati wa kurarua na wakati wa kushona,

8wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia,

9Mfanyakazi anapata faida gani kutokana na taabu yake?

10Nimeona mzigo Mungu alioweka juu ya wanadamu.

11Amefanya kila kitu kiwe kizuri kwa wakati wake. Pia ameiweka hiyo milele katika mioyo ya wanadamu, wala hawawezi kutambua kwa kina yale ambayo Mungu amefanya tangu mwanzo hadi mwisho.

12Ninajua kwamba hakuna kitu bora kwa wanadamu kuliko kuwa na furaha na kutenda mema wakati wanapoishi.

13Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote.

14Ninajua kwamba kila kitu anachokifanya Mungu kitadumu milele, hakuna kinachoweza kuongezwa au kupunguzwa. Mungu hufanya hivyo ili watu wamche yeye.

15Chochote kilichopo kilishakuwepo,

16Pia nikaona kitu kingine tena chini ya jua:

17Nikafikiri moyoni mwangu,

18Pia nikafikiri, “Kuhusu wanadamu, Mungu huwajaribu ili wajione kwamba wao ni kama wanyama.

19Hatima ya mwanadamu ni kama ile ya wanyama; wote wana mwisho unaofanana: Jinsi anavyokufa mnyama, ndivyo anavyokufa mwanadamu. Wote wana pumzi inayofanana; mwanadamu hana cha zaidi kuliko mnyama. Kila kitu ni ubatili.

20Wote huenda mahali panapofanana; wote hutoka mavumbini, mavumbini wote hurudi.

21Ni nani ajuaye kama roho ya mtu huenda juu na roho ya mnyama hushuka chini ardhini?”

22Kwa hiyo nikaona kwamba hakuna kitu kilicho bora zaidi kwa mwanadamu kuliko kuifurahia kazi yake, kwa sababu hilo ndilo fungu lake. Kwa maana ni nani awezaye kumrudisha ili aje kuona kile kitakachotendeka baada yake?

← Mhubiri 2 Mhubiri Mhubiri 4 →