We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

2 Samweli 23

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← 2 Samweli 22 2 Samweli 2 Samweli 24 →

1Haya ni maneno ya mwisho ya Daudi:

2“Roho wa Bwana alinena kupitia kwangu,

3Mungu wa Israeli alinena,

4yeye ni kama mwanga wa asubuhi jua lichomozapo

5“Je, si hivyo ilivyo nyumba yangu

6Lakini watu waovu wote

7Yeyote agusaye miiba

8Haya ndiyo majina ya mashujaa wa Daudi:

9Wa pili wake alikuwa Eleazari mwana wa Dodai,23:9 Dodai tafsiri nyingine zinamwita Dodo. Mwahohi. Akiwa mmojawapo wa wale mashujaa watatu, alikuwa pamoja na Daudi wakati waliwadhihaki Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko Pas-Damimu kwa ajili ya vita. Kisha watu wa Israeli wakarudi nyuma,

10lakini yeye alisimama imara akawaua Wafilisti hadi mkono wake ukachoka na ukagandamana na upanga. Bwana akawapa ushindi mkubwa siku ile. Vikosi vikarudi kwa Eleazari, kuteka tu nyara za waliokufa.

11Aliyefuata alikuwa Shama mwana wa Agee, Mharari. Wafilisti walipokusanyika pamoja mahali palipokuwa shamba lililojaa dengu, vikosi vya Israeli viliwakimbia.

12Lakini Shama akasimama imara katikati ya lile shamba. Akalitetea na kuwaua Wafilisti, naye Bwana akawapa ushindi mkubwa.

13Wakati wa mavuno, viongozi watatu kati ya viongozi thelathini walishuka, wakamwendea Daudi katika pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai.

14Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome, na kambi ya Wafilisti ilikuwa huko Bethlehemu.

15Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu!”

16Basi mashujaa hao watatu wakapenya katikati ya Wafilisti, wakaenda kuchota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini Daudi akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Bwana.

17Akasema, “Iwe mbali nami, Ee Bwana, kufanya kitu hiki. Je, hii si damu ya watu ambao walikwenda kwa kuhatarisha maisha yao?” Naye Daudi hakuyanywa.

18Abishai ndugu yake Yoabu mwana wa Seruya ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300 ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu.

19Je, hakupata heshima kubwa zaidi kuliko hao Watatu? Alikuwa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao.

20Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba.

21Pia alimuua Mmisri mrefu mkubwa. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki mkononi mwake, Benaya alimwendea akiwa na rungu. Alipokonya mkuki kutoka mkononi mwa Mmisri na kumuua kwa mkuki wake mwenyewe.

22Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu.

23Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu. Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake.

24Miongoni mwa wale Thelathini walikuwepo:

25Shama, Mharodi;

26Helesi, Mpalti;

27Abiezeri kutoka Anathothi;

28Salmoni, Mwahohi;

29Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi;

30Benaya Mpirathoni;

31Abi-Alboni, Mwaribathi;

32Eliaba, Mshaalboni;

33mwana wa Shama, Mharari;

34Elifeleti mwana wa Ahasbai, Mmaakathi;

35Hezro, Mkarmeli;

36Igali mwana wa Nathani kutoka Soba;

37Seleki, Mwamoni;

38Ira, Mwithiri;

39na Uria, Mhiti.

← 2 Samweli 22 2 Samweli 2 Samweli 24 →