1Benyamini akamzaa: Bela mzaliwa wake wa kwanza,
2Noha mwanawe wa nne na Rafa mwanawe wa tano.
3Wana wa Bela walikuwa:
4Abishua, Naamani, Ahoa,
5Gera, Shefufani na Huramu.
6Hawa ndio wazao wa Ehudi, waliokuwa viongozi wa jamaa za wale walioishi huko Geba na ambao walihamishiwa Manahathi:
7Naamani, Ahiya na Gera. Gera alikuwa baba yao Uza na Ahihudi na ndiye aliwaongoza kwenda uhamishoni.
8Shaharaimu aliwazaa wana katika nchi ya Moabu baada ya kuwapa talaka wake zake wawili yaani, Hushimu na Baara.
9Kwa mkewe Hodeshi, akawazaa wana saba: Yobabu, Sibia, Mesha, Malkamu,
10Yeuzi, Sakia na Mirma. Hawa ndio waliokuwa wanawe, viongozi wa jamaa zao.
11Hushimu alimzalia: Abitubu na Elpaali.
12Wana wa Elpaali walikuwa:
13na Beria na Shema, waliokuwa viongozi wa zile jamaa zilizokuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na ambao waliwafukuza wenyeji wa Gathi.
14Wana wa Beria walikuwa Ahio, Shashaki, Yeremothi,
15Zebadia, Aradi, Ederi,
16Mikaeli, Ishpa, na Yoha.
17Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi,
18Ishmerai, Izlia na Yobabu ndio waliokuwa wana wa Elpaali.
19Yakimu, Zikri, Zabdi,
20Elienai, Silethai, Elieli,
21Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wana wa Shimei.
22Wana wa Shashaki walikuwa Ishpani, Eberi, Elieli,
23Abdoni, Zikri, Hanani,
24Hanania, Elamu, Anthothiya,
25Ifdeya na Penueli.
26Shamsherai, Sheharia, Athalia,
27Yaareshia, Eliya na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu.
28Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao wakuu, kama ilivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.
29Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni.
30Mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu,
31Gedori, Ahio, Zekeri,
32na Miklothi ambaye alikuwa baba yake Shimea. Hawa pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu.
33Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli, Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali.
34Yonathani akamzaa:
35Wana wa Mika walikuwa:
36Ahazi akamzaa Yehoada. Naye Yehoada akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa.
37Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Rafa, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli.
38Aseli alikuwa na wana sita; haya ndiyo majina yao:
39Wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa:
40Wana wa Ulamu walikuwa mashujaa hodari walioweza kutumia upinde. Alikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla yao 150.