We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

1 Nyakati 6

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← 1 Nyakati 5 1 Nyakati 1 Nyakati 7 →

1Wana wa Lawi walikuwa:

2Wana wa Kohathi walikuwa:

3Amramu alikuwa na wana:

4Eleazari akamzaa Finehasi,

5Abishua akamzaa Buki,

6Uzi akamzaa Zerahia,

7Merayothi akamzaa Amaria,

8Ahitubu akamzaa Sadoki,

9Ahimaasi akamzaa Azaria,

10Yohanani akamzaa Azaria (ndiye alifanya kazi ya ukuhani katika Hekalu alilojenga Mfalme Solomoni huko Yerusalemu),

11Azaria akamzaa Amaria,

12Ahitubu akamzaa Sadoki,

13Shalumu akamzaa Hilkia,

14Azaria akamzaa Seraya,

15Yehosadaki alihamishwa wakati Bwana aliwapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Mfalme Nebukadneza.

16Wana wa Lawi walikuwa:

17Haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni:

18Wana wa Kohathi walikuwa:

19Wana wa Merari walikuwa:

20Wazao wa Gershoni:

21Zima akamzaa Yoa,

22Wazao wa Kohathi:

23Asiri akamzaa Elikana,

24Asiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli,

25Wazao wa Elikana walikuwa:

26Ahimothi akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Sofai,

27Nahathi akamzaa Eliabu,

28Wana wa Samweli walikuwa:

29Wafuatao ndio wazao wa Merari:

30Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia,

31Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Bwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko.

32Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

33Wafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao:

34mwana wa Elikana, mwana wa Yerohamu,

35mwana wa Sufu, mwana wa Elikana,

36mwana wa Elikana, mwana wa Yoeli,

37mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri,

38mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi,

39na msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume:

40mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya,

41mwana wa Ethni,

42mwana wa Ethani, mwana wa Zima,

43mwana wa Yahathi,

44Na kutoka kwa walioshirikiana nao, Wamerari, mkono wake wa kushoto:

45mwana wa Hashabia,

46mwana wa Amsi, mwana wa Bani,

47mwana wa Mahli,

48Ndugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu.

49Lakini Aroni na uzao wake ndio waliokuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Mose mtumishi wa Mungu.

50Hawa ndio waliokuwa wazao wa Aroni:

51Abishua akamzaa Buki,

52Zerahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria,

53Ahitubu akamzaa Sadoki,

54Zifuatazo ni sehemu walizopewa ziwe nchi yao kwa ajili ya makazi yao (walipewa wazao wa Aroni waliotoka katika ukoo wa Wakohathi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):

55Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda pamoja na sehemu ya malisho inayouzunguka.

56Lakini mashamba pamoja na vijiji vilivyouzunguka mji alipewa Kalebu mwana wa Yefune.

57Kwa hiyo wazao wa Aroni walipewa miji ifuatayo pamoja na eneo la malisho: Hebroni (mji wa makimbilio), Libna, Yatiri, Eshtemoa,

58Hileni, Debiri,

59Ashani, Yuta na Beth-Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho.

60Kutoka kabila la Benyamini walipewa Gibeoni, Geba, Alemethi na Anathothi, pamoja na maeneo yake ya malisho.

61Wazao waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za nusu ya kabila la Manase.

62Wazao wa Gershoni, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na mitatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.

63Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.

64Kwa hiyo Waisraeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yake ya malisho.

65Kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini walipewa miji iliyotajwa hapo juu.

66Baadhi ya koo za Wakohathi walipewa kama nchi yao miji kutoka kabila la Efraimu.

67Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji wa makimbilio) na Gezeri,

68Yokmeamu, Beth-Horoni,

69Aiyaloni na Gath-Rimoni, pamoja na maeneo yake ya malisho.

70Kutoka nusu ya kabila la Manase, Waisraeli waliwapa koo za Wakohathi waliobaki miji ya Aneri na Bileamu pamoja na maeneo yake ya malisho.

71Wagershoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho:

72Kutoka kabila la Isakari

73Ramothi na Anemu, pamoja na maeneo yake ya malisho.

74Kutoka kabila la Asheri

75Hukoki na Rehobu, pamoja na maeneo yake ya malisho.

76Kutoka kabila la Naftali

77Wamerari (Walawi waliobakia) walipokea miji ifuatayo:

78Kutoka kabila la Reubeni, ngʼambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko

79Kedemothi na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho.

80Na kutoka kabila la Gadi

81Heshboni na Yazeri, pamoja na maeneo yake ya malisho.

← 1 Nyakati 5 1 Nyakati 1 Nyakati 7 →