We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

1 Nyakati 16

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← 1 Nyakati 15 1 Nyakati 1 Nyakati 17 →

1Wakaleta Sanduku la Mungu na kuliweka ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, na wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu.

2Baada ya Daudi kumaliza kutoa hizo sadaka za kuteketezwa na hizo sadaka za amani, akawabariki watu katika jina la Bwana.

3Kisha akamgawia kila Mwisraeli mwanaume na mwanamke mkate, andazi la tende na andazi la zabibu kavu.

4Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku la Bwana kufanya maombi, kumshukuru na kumsifu Bwana, Mungu wa Israeli:

5Asafu ndiye alikuwa mkuu wao, akisaidiwa na Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaya, Obed-Edomu na Yeieli. Hawa ndio wangepiga zeze na vinubi, Asafu angepiga matoazi,

6nao Benaya na Yahazieli makuhani, ndio wangepiga tarumbeta mara kwa mara mbele ya Sanduku la Agano la Mungu.

7Siku ile, kitu cha kwanza Daudi alichofanya ni kumkabidhi Asafu na wenzake zaburi hii ya shukrani kwa Bwana:

8Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake;

9Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa;

10Lishangilieni jina lake takatifu;

11Mtafuteni Bwana na nguvu zake;

12Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya,

13enyi wazao wa Israeli mtumishi wake,

14Yeye ndiye Bwana Mungu wetu;

15Hulikumbuka agano lake milele,

16agano alilolifanya na Abrahamu,

17Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri,

18“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani

19Walipokuwa wachache kwa idadi,

20walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine,

21Hakuruhusu mtu yeyote awaonee;

22“Msiwaguse niliowatia mafuta;

23Mwimbieni Bwana dunia yote;

24Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa,

25Kwa kuwa Bwana ni mkuu,

26Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu,

27Fahari na enzi viko mbele yake;

28Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa,

29mpeni Bwana utukufu

30Dunia yote na itetemeke mbele zake!

31Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi;

32Bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;

33Kisha miti ya msituni itaimba,

34Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema;

35Mlilieni, “Ee Mungu Mwokozi wetu, tuokoe.

36Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli,

37Daudi akamwacha Asafu na wenzake mbele ya Sanduku la Agano la Bwana ili wahudumu humo mara kwa mara, kulingana na mahitaji ya kila siku.

38Pia akamwacha Obed-Edomu pamoja na wenzake sitini na wanane wahudumu pamoja nao. Obed-Edomu mwana wa Yeduthuni na pia Hosa walikuwa mabawabu wa lango.

39Daudi akamwacha kuhani Sadoki pamoja na makuhani wenzake mbele ya hema ya ibada ya Bwana katika mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni

40ili kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Bwana kwenye madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mara kwa mara, asubuhi na jioni, sawasawa na kila kitu kilichoandikwa katika sheria ya Bwana ambayo alikuwa amempa Israeli.

41Waliohudumu pamoja nao walikuwa Hemani, Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa na kutajwa kwa jina kumpa Bwana shukrani, “Kwa maana fadhili zake zadumu milele.”

42Hemani na Yeduthuni walikuwa na wajibu wa kupiga tarumbeta, matoazi na kutumia vyombo vingine kwa ajili ya nyimbo za sifa kwa Mungu. Wana wa Yeduthuni waliwekwa langoni.

43Kisha watu wote wakaondoka, kila mmoja akarudi nyumbani kwake, naye Daudi akarudi nyumbani kuibariki jamaa yake.

← 1 Nyakati 15 1 Nyakati 1 Nyakati 17 →