We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

Hesabu 26

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← Hesabu 25 Hesabu Hesabu 27 →

1Baada ya hiyo tauni, Bwana akamwambia Mose na Eleazari mwana wa kuhani Aroni,

2“Hesabu jumuiya yote ya Kiisraeli kwa jamaa zao, wale wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, ambao wanaweza kutumika katika jeshi la Israeli.”

3Hivyo Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya Moabu, ngʼambo ya Yordani kutokea Yeriko, wakasema,

4“Hesabuni wanaume wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kama Bwana alivyomwagiza Mose.”

5Wazao wa Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa:

6kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni;

7Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa 43,730.

8Mwana wa Palu alikuwa Eliabu,

9nao wana wa Eliabu walikuwa Nemueli, Dathani na Abiramu. Hawa wawili Dathani na Abiramu ndio walikuwa maafisa wa jumuiya ambao walimwasi Mose na Aroni, na walikuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora wakati walimwasi Bwana.

10Ardhi ilifunua kinywa chake na kuwameza pamoja na Kora, ambaye wafuasi wake walikufa wakati moto ulipowateketeza wanaume 250. Nao walikuwa kama alama ya onyo.

11Pamoja na hayo, hao ukoo wa Kora hawakufa.

12Wazao wa Simeoni kwa koo zao walikuwa:

13kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera;

14Hizi ndizo koo za Simeoni; walikuwa 22,200.

15Wazao wa Gadi kwa koo zao walikuwa:

16kutoka kwa Ozni, ukoo wa Waozni;

17kutoka kwa Arodi, ukoo wa Waarodi;

18Hizi ndizo zilizokuwa koo za Gadi; wale waliohesabiwa walikuwa 40,500.

19Eri na Onani walikuwa wana wa Yuda, lakini walifia huko Kanaani.

20Wazao wa Yuda kwa koo zao walikuwa:

21Wazao wa Peresi walikuwa:

22Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda; wale waliohesabiwa walikuwa 76,500.

23Wazao wa Isakari kwa koo zao walikuwa:

24kutoka kwa Yashubu, ukoo wa Wayashubu;

25Hizi ndizo zilizokuwa koo za Isakari; wale waliohesabiwa walikuwa 64,300.

26Wazao wa Zabuloni kwa koo zao walikuwa:

27Hizi ndizo zilizokuwa koo za Zabuloni, wale waliohesabiwa walikuwa 60,500.

28Wazao wa Yosefu kwa koo zao kutoka kwa Manase na kwa Efraimu walikuwa:

29Wazao wa Manase:

30Hawa ndio waliokuwa wazao wa Gileadi:

31kutoka kwa Asirieli, ukoo wa Waasirieli;

32kutoka kwa Shemida, ukoo wa Washemida;

33(Selofehadi mwana wa Heferi hakuzaa wana, bali alikuwa na watoto wa kike tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.)

34Hizi ndizo zilizokuwa koo za Manase; wale waliohesabiwa walikuwa 52,700.

35Hawa walikuwa wazao wa Efraimu kwa koo zao:

36Hawa ndio walikuwa wazao wa Shuthela:

37Hizi ndizo zilizokuwa koo za Efraimu; wale waliohesabiwa walikuwa 32,500.

38Wazao wa Benyamini kwa koo zao walikuwa:

39kutoka kwa Shufamu, ukoo wa Washufamu;

40Wazao wa Bela kutoka kwa Ardi na Naamani walikuwa:

41Hizi ndizo zilizokuwa koo za Benyamini; wale waliohesabiwa walikuwa 45,600.

42Hawa ndio waliokuwa wazao wa Dani kwa koo zao:

43Wote walikuwa koo za Washuhamu; wale waliohesabiwa walikuwa 64,400.

44Wazao wa Asheri kwa koo zao walikuwa:

45kutoka kwa wazao wa Beria:

46(Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera.)

47Hizi ndizo zilizokuwa koo za Asheri; wale waliohesabiwa walikuwa 53,400.

48Wazao wa Naftali kwa koo zao walikuwa:

49kutoka kwa Yeseri, ukoo wa Wayeseri;

50Hizi ndizo zilizokuwa koo za Naftali; wale waliohesabiwa walikuwa 45,400.

51Jumla ya hesabu ya wanaume wa Israeli ilikuwa 601,730.

52Bwana akamwambia Mose,

53“Watagawiwa nchi kama urithi kwa kulingana na hesabu ya majina.

54Kundi kubwa zaidi lipe urithi mkubwa zaidi, na kundi dogo zaidi lipewe urithi mdogo zaidi; kila kundi litapokea urithi wake kulingana na hesabu ya wale walioorodheshwa.

55Hakikisha kuwa nchi inagawanywa kwa kura. Kile kitakachorithiwa na kila kikundi kitakuwa kwa kulingana na majina ya kabila la babu yao.

56Kila urithi utagawanywa kwa kura miongoni mwa makundi makubwa na madogo.”

57Hawa walikuwa Walawi ambao walihesabiwa kwa koo zao:

58Hizi pia zilikuwa koo za Walawi:

59jina la mke wa Amramu ni Yokebedi, naye pia alikuwa mzao wa Lawi, ambaye alizaliwa kwa Walawi nchini Misri. Alimzalia Amramu: Aroni, Mose na dada yao Miriamu.

60Aroni alikuwa baba yake Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari.

61Lakini Nadabu na Abihu walikufa wakati walitoa sadaka mbele za Bwana kwa moto usioruhusiwa.)

62Wanaume wote wa Walawi wa umri wa mwezi mmoja na zaidi walikuwa 23,000. Wao hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine kwa sababu hawakupokea urithi miongoni mwao.

63Hawa ndio walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari wakati waliwahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko.

64Hakuna hata mmoja wao aliyekuwa miongoni mwa wale waliohesabiwa na Mose na kuhani Aroni wakati waliwahesabu Waisraeli katika Jangwa la Sinai.

65Kwa maana Bwana alikuwa amewaambia hao Waisraeli hakika wangekufa huko jangwani, wala hakuna mmoja wao aliyeachwa, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni.

← Hesabu 25 Hesabu Hesabu 27 →