We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

Hesabu 24

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← Hesabu 23 Hesabu Hesabu 25 →

1Basi Balaamu alipoona imempendeza Bwana kubariki Israeli, hakuendelea tena kutafuta uchawi kama nyakati nyingine, bali aligeuza uso wake kuelekea nyikani.

2Balaamu alipotazama nje na kuona Israeli amepiga kambi kabila kwa kabila, Roho wa Mungu akawa juu yake,

3naye akatoa ujumbe wake:

4ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu,

5“Tazama jinsi yalivyo mazuri mahema yako, ee Yakobo,

6“Kama mabonde, yanaenea,

7Maji yatatiririka kutoka ndoo zake;

8“Mungu alimleta kutoka Misri;

9Hujikunyata na kuvizia kama simba,

10Ndipo hasira ya Balaki ikawaka dhidi ya Balaamu. Akapiga mikono yake pamoja, akamwambia Balaamu, “Nilikuita uje kuwalaani adui zangu, lakini umewabariki mara hizi tatu.

11Sasa ondoka upesi uende nyumbani! Mimi nilisema nitakuzawadia vizuri sana, lakini Bwana amekuzuia usizawadiwe.”

12Balaamu akamwambia Balaki, “Je, hukumbuki jinsi nilivyowaambia wajumbe uliowatuma kwangu? Niliwaambia hivi,

13‘Hata ikiwa Balaki angenipa jumba lake la kifalme likiwa limejazwa fedha na dhahabu, nisingeweza kufanya kitu chochote kwa matakwa yangu, kikiwa kizuri au kibaya, kwenda kinyume na agizo la Bwana, nami imenipasa kusema tu kile Bwana atakachosema’?

14Sasa ninarudi kwa watu wangu. Lakini njoo, nikuonye kuhusu kile watu hawa watakachowatenda watu wako siku zijazo.”

15Kisha Balaamu akatoa ujumbe wake:

16ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu,

17“Namwona yeye, lakini si sasa;

18Edomu itamilikiwa,

19Mtawala atakuja kutoka kwa Yakobo

20Kisha Balaamu akawaona watu wa Amaleki, na kutoa ujumbe wake:

21Kisha akawaona Wakeni, akatoa ujumbe wake:

22Hata hivyo ninyi Wakeni mtaangamizwa

23Ndipo akatoa ujumbe wake:

24Meli zitakuja kutoka pwani za Kitimu,

25Kisha Balaamu akainuka na kurudi nyumbani kwake, naye Balaki akashika njia yake.

← Hesabu 23 Hesabu Hesabu 25 →