We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

Nehemia 7

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← Nehemia 6 Nehemia Nehemia 8 →

1Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na nikaweka milango, mabawabu wa lango, waimbaji, na Walawi waliteuliwa.

2Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine.

3Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”

4Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu.

5Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:

6Hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,

7wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana):

8wazao wa Paroshi

9wazao wa Shefatia

10wazao wa Ara

11wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu)

12wazao wa Elamu

13wazao wa Zatu

14wazao wa Zakai

15wazao wa Binui

16wazao wa Bebai

17wazao wa Azgadi

18wazao wa Adonikamu

19wazao wa Bigwai

20wazao wa Adini

21wazao wa Ateri (kupitia Hezekia)

22wazao wa Hashumu

23wazao wa Besai

24wazao wa Harifu

25wazao wa Gibeoni

26watu wa Bethlehemu na Netofa

27watu wa Anathothi

28watu wa Beth-Azmawethi

29watu wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi

30watu wa Rama na Geba

31watu wa Mikmashi

32watu wa Betheli na Ai

33watu wa Nebo

34wazao wa Elamu

35wazao wa Harimu

36wazao wa Yeriko

37wazao wa Lodi, Hadidi na Ono

38wazao wa Senaa

39Makuhani:

40wazao wa Imeri

41wazao wa Pashuri

42wazao wa Harimu

43Walawi:

44Waimbaji:

45Mabawabu wa malango:

46Watumishi wa Hekalu:7:46 Yaani Wanethini (pia 7:60, 73).

47wazao wa Kerosi, Sia, Padoni,

48wazao wa Lebana, Hagaba, Shalmai,

49wazao wa Hanani, Gideli, Gahari,

50wazao wa Reaya, Resini, Nekoda,

51wazao wa Gazamu, Uza, Pasea,

52wazao wa Besai, Meunimu, Nefusimu,

53wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,

54wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,

55wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,

56wazao wa Nesia na Hatifa.

57Wazao wa watumishi wa Solomoni:

58wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,

59wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Amoni.

60Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni

61Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:

62wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda

63Na kutoka miongoni mwa makuhani:

64Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.

65Kwa hiyo, mtawala7:65 Au Tirshatha: jina la heshima aliloitwa mtawala wa Yuda chini ya Ufalme wa Uajemi (pia 7:70). aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.7:65 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.

66Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360;

67tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 245.

68Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245

69ngamia 435 na punda 6,720.

70Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,0007:70 Darkoni 1,000 za dhahabu ni sawa na uzito wa kilo 8.6. za dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani.

71Baadhi ya viongozi wa jamaa walikabidhi kwenye hazina darkoni 20,000 za dhahabu,7:71 Darkoni 20,000 za dhahabu ni sawa na kilo 172. na mane 2,2007:71 Mane 2,200 za fedha ni sawa na kilo 1,300. za fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

72Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni 20,000 za dhahabu, mane 2,000 za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani.

73Makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji na watumishi wa Hekalu, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao wenyewe.

← Nehemia 6 Nehemia Nehemia 8 →