1Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato akiwa mtawala wa Uyahudi, Herode akiwa mfalme wa Galilaya, Filipo ndugu yake akiwa mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania akiwa mfalme wa Abilene,
2nao Anasi na Kayafa wakiwa makuhani wakuu, neno la Mungu likamjia Yohana, mwana wa Zekaria huko jangwani.
3Akaenda katika nchi yote kandokando ya Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi.
4Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya:
5Kila bonde litajazwa,
6Nao watu wote watauona
7Yohana akauambia ule umati wa watu uliokuwa unakuja ili kubatizwa naye, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja?
8Basi zaeni matunda yastahiliyo toba. Wala msianze kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Abrahamu, baba yetu.’ Kwa maana nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Abrahamu watoto kutoka mawe haya.
9Hata sasa shoka limeshawekwa tayari kwenye shina la kila mti. Basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.”
10Ule umati wa watu ukamuuliza, “Inatupasa tufanyeje basi?”
11Yohana akawaambia, “Aliye na kanzu mbili amgawie asiye nayo, naye aliye na chakula na afanye vivyo hivyo.”
12Watoza ushuru nao wakaja ili wabatizwe, wakamuuliza, “Bwana na sisi inatupasa tufanyeje?”
13Akawaambia, “Msichukue zaidi ya kiwango mlichopangiwa.”
14Askari nao wakamuuliza, “Je, nasi inatupasa tufanye nini?”
15Watu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wanajiuliza mioyoni mwao iwapo Yohana angeweza kuwa ndiye Kristo.3:15 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
16Yohana akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji.3:16 Tafsiri nyingine zinasema ndani ya maji. Lakini atakuja aliye na nguvu kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
17Pepeto lake liko mkononi, tayari kusafisha sakafu yake ya kupuria na kuikusanya ngano ghalani, lakini makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.”
18Basi, kwa maonyo mengine mengi Yohana aliwasihi na kuwahubiria watu Habari Njema.
19Lakini Yohana alipomkemea Mfalme Herode kuhusu uhusiano wake na Herodia, mke wa ndugu yake, na maovu mengine aliyokuwa amefanya,
20Herode aliongezea jambo hili kwa hayo mengine yote: alimfunga Yohana gerezani.
21Baada ya watu wote kubatizwa, Yesu naye akabatizwa. Naye alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka.
22Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa umbo kama la hua, nayo sauti kutoka mbinguni ikasema: “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.”
23Yesu alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza huduma yake. Alikuwa akidhaniwa kuwa mwana wa Yosefu,
24Eli alikuwa mwana wa Mathati,
25Yosefu alikuwa mwana wa Matathia,
26Nagai alikuwa mwana wa Maathi,
27Yoda alikuwa mwana wa Yoanani,
28Neri alikuwa mwana wa Melki,
29Eri alikuwa mwana wa Yoshua,
30Lawi alikuwa mwana wa Simeoni,
31Melea alikuwa mwana wa Mena,
32Daudi alikuwa mwana wa Yese,
33Nashoni alikuwa mwana wa Aminadabu,
34Yuda alikuwa mwana wa Yakobo,
35Nahori alikuwa mwana wa Serugi,
36Sala alikuwa mwana wa Kenani,
37Lameki alikuwa mwana wa Methusela,
38Kenani alikuwa mwana wa Enoshi,