We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

Ayubu 42

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← Ayubu 41 Ayubu

1Ndipo Ayubu akamjibu Bwana:

2“Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote,

3Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’

4“Ulisema, ‘Sikiliza sasa, nami nitanena;

5Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako,

6Kwa hiyo najidharau mwenyewe,

7Baada ya Bwana kusema mambo haya yote na Ayubu, akamwambia Elifazi Mtemani, “Nina hasira juu yako na juu ya rafiki zako wawili, kwa sababu hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.

8Basi sasa chukueni mafahali saba na kondoo dume saba mkamwendee mtumishi wangu Ayubu nanyi mkatoe sadaka za kuteketezwa kwa ajili yenu wenyewe. Mtumishi wangu Ayubu ataomba kwa ajili yenu, nami nitayakubali maombi yake ili nisiwatendee sawasawa na upumbavu wenu. Ninyi hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.”

9Kwa hiyo Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi wakafanya kama Bwana alivyowaambia; naye Bwana akayakubali maombi ya Ayubu.

10Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake, Bwana akamwondoa kwenye uteka, akamfanikisha tena naye akampa mara mbili ya vile alivyokuwa navyo hapo mwanzoni.

11Ndipo ndugu zake wote waume kwa wake na kila mtu aliyemfahamu mwanzoni, wakaja wakala pamoja naye katika nyumba yake. Wakamfariji na kumtuliza moyo juu ya taabu yote Bwana aliyoileta juu yake, nao kila mmoja akampa kipande cha fedha na pete ya dhahabu.

12Bwana akaibariki sehemu ya mwisho ya maisha ya Ayubu kuliko ile ya kwanza. Alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, ngamia elfu sita, jozi za mafahali elfu moja, na punda wa kike elfu moja.

13Tena alikuwa na wana saba na binti watatu.

14Binti wa kwanza aliitwa Yemima, wa pili Kesia na wa tatu Keren-Hapuki.

15Hapakuwepo mahali popote katika nchi ile yote palipopatikana wanawake wazuri kama binti za Ayubu; naye baba yao akawapa urithi pamoja na ndugu zao.

16Baada ya hili Ayubu akaishi miaka 140; akawaona wanawe na wana wa wanawe hata kizazi cha nne.

17Hivyo Ayubu akafa, akiwa mzee aliyekuwa ameshiba siku.

← Ayubu 41 Ayubu