1Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:
2Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.
3Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi12:3 Yaani Bahari ya Galilaya. hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi12:3 Yaani Bahari Mfu.), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.
4Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.
5Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.
6Mose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.
7Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao:
8nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):
9mfalme wa Yeriko
10mfalme wa Yerusalemu
11mfalme wa Yarmuthi
12mfalme wa Egloni
13mfalme wa Debiri
14mfalme wa Horma
15mfalme wa Libna
16mfalme wa Makeda
17mfalme wa Tapua
18mfalme wa Afeki
19mfalme wa Madoni
20mfalme wa Shimron-Meroni
21mfalme wa Taanaki
22mfalme wa Kedeshi
23mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori) 12:23 Au: katika miinuko ya Nafoth-Dori.
24mfalme wa Tirsa