1“Lakini Ayubu, sasa, sikiliza maneno yangu;
2Karibu nitafungua kinywa changu;
3Maneno yangu yanatoka katika moyo mnyofu;
4Roho wa Mungu ameniumba;
5Unijibu basi, kama unaweza;
6Mimi ni kama wewe mbele za Mungu;
7Huna sababu ya kuniogopa,
8“Lakini umesema nikiwa ninakusikia,
9‘Mimi ni safi na sina dhambi;
10Lakini bado Mungu amepata dosari kwangu,
11Ananifunga miguu kwa pingu,
12“Lakini mimi ninakuambia, katika jambo hili wewe una makosa,
13Kwa nini unamlalamikia
14Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja,
15Mungu husema na mwanadamu katika ndoto,
16anaweza akasemea masikioni mwao,
17ili kumgeuza mtu kutoka kwenye kutenda mabaya
18kuiokoa nafsi yake na shimo,
19Mtu anaweza kutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake,
20kiasi kwamba maisha yake yenyewe yanakataa chakula
21Nyama ya mwili wake huisha kwa kukonda,
22Nafsi yake inakaribia kaburi,
23“Kama bado kuna malaika upande wake
24kumwonea huruma na kusema,
25ndipo nyama ya mwili wake hufanywa mpya kama ya mtoto;
26Humwomba Mungu, akapata kibali kwake,
27Ndipo huja mbele za watu na kusema,
28Alinikomboa nafsi yangu nisitumbukie shimoni,
29“Mungu hufanya haya yote kwa mwanadamu;
30ili aigeuze nafsi yake toka shimoni,
31“Ayubu, zingatia, nisikilize mimi;
32Kama unalo lolote la kusema, unijibu;
33Lakini kama huna la kusema, basi nisikilize mimi;