We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

Isaya 38

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← Isaya 37 Isaya Isaya 39 →

1Katika siku hizo Hezekia akaugua, naye akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akaenda kwake na kumwambia, “Hili ndilo asemalo Bwana: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”

2Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana:

3“Ee Bwana, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote, na kufanya yaliyo mema machoni pako.” Naye Hezekia akalia kwa uchungu.

4Ndipo neno la Bwana likamjia Isaya, kusema:

5“Nenda ukamwambie Hezekia, ‘Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa baba yako Daudi: Nimeyasikia maombi yako na nimeona machozi yako. Nitakuongezea miaka kumi na mitano katika maisha yako.

6Nami nitakuokoa wewe pamoja na mji huu mkononi mwa mfalme wa Ashuru. Nitaulinda mji huu.

7“ ‘Hii ndiyo ishara ya Bwana kwako ya kwamba Bwana atafanya kile alichoahidi:

8Nitafanya kivuli cha jua kwenye ngazi iliyojengwa na Ahazi kirudi nyuma madaraja kumi.’ ” Hivyo jua likarudi nyuma madaraja kumi ambayo lilikuwa limeshuka.

9Maandiko ya Hezekia mfalme wa Yuda baada ya kuugua kwake na kupona:

10Nilisema, “Katika ustawi wa maisha yangu,

11Nilisema, “Sitamwona tena Bwana,

12Kama hema la mchunga mifugo,

13Nilingoja kwa uvumilivu hadi mapambazuko,

14Nililia kama mbayuwayu au korongo,

15Lakini niseme nini?

16Bwana, kwa mambo kama haya watu huishi,

17Hakika ilikuwa ya faida yangu

18Kwa maana kaburi38:18 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. haliwezi kukusifu,

19Walio hai, walio hai: hao wanakusifu,

20Bwana ataniokoa,

21Isaya alikuwa amesema, “Tengenezeni dawa ya kubandika ya tini, mweke juu ya jipu, naye atapona.”

22Hezekia alikuwa ameuliza, “Kutakuwa na ishara gani kwamba nitapanda kwenda Hekalu la Bwana?”

← Isaya 37 Isaya Isaya 39 →