1Zamani Mungu alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali,
2lakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kwa njia ya Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kupitia kwake aliuumba ulimwengu.
3Mwana ni mngʼao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Aliye Mkuu huko mbinguni.
4Kwa hiyo alifanyika bora kuliko malaika, kama jina alilorithi lilivyo bora kuliko lao.
5Kwa maana ni malaika yupi ambaye wakati wowote Mungu alipata kumwambia,
6Tena, Mungu amletapo mzaliwa wake wa kwanza ulimwenguni, anasema,
7Anenapo kuhusu malaika asema,
8Lakini kwa habari za Mwana asema,
9Umependa haki na kuchukia uovu;
10Pia asema,
11Hizo zitatoweka, lakini wewe utadumu;
12Utazikungʼutakungʼuta kama joho,
13Je, ni kwa malaika yupi ambaye Mungu amepata kumwambia wakati wowote,
14Je, malaika wote si roho watumikao, waliotumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu?