We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

Mwanzo 46

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← Mwanzo 45 Mwanzo Mwanzo 47 →

1Hivyo Israeli akaondoka na vyote vilivyokuwa mali yake, naye alipofika Beer-Sheba, akamtolea dhabihu Mungu wa Isaki baba yake.

2Mungu akanena na Israeli katika maono usiku na kusema, “Yakobo! Yakobo!”

3Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa baba yako, usiogope kushuka Misri, kwa maana huko nitakufanya taifa kubwa.

4Nitashuka Misri pamoja nawe, nami hakika nitakurudisha tena Kanaani. Mikono ya Yosefu mwenyewe ndiyo itakayofunga macho yako.”

5Ndipo Yakobo akaondoka Beer-Sheba nao wana wa Israeli wakamchukua baba yao Yakobo na watoto wao na wake zao katika magari ya kukokotwa yale Farao aliyokuwa amempelekea kumsafirisha.

6Wakachukua pia mifugo yao na mali walizokuwa wamezipata Kanaani, Yakobo na uzao wake wote wakashuka Misri.

7Akawachukua wanawe na binti zake, wajukuu wake wa kiume na wa kike, yaani uzao wake wote mpaka Misri.

8Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli (Yakobo na wazao wake), waliokwenda Misri:

9Wana wa Reubeni ni:

10Wana wa Simeoni ni:

11Wana wa Lawi ni:

12Wana wa Yuda ni:

13Wana wa Isakari ni:

14Wana wa Zabuloni ni:

15Hawa ndio wana wa Lea aliomzalia Yakobo huko Padan-Aramu pamoja na binti yake Dina. Jumla ya wanawe na binti zake walikuwa thelathini na watatu.

16Wana wa Gadi ni:

17Wana wa Asheri ni:

18Hawa ndio watoto Zilpa aliomzalia Yakobo, ambao Labani alimpa binti yake Lea; jumla yao walikuwa kumi na sita.

19Wana wa Raheli mke wa Yakobo ni:

20Huko Misri, Asenathi binti wa Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni,46:20 Yaani Heliopoli (Mji wa Jua). alimzalia Yosefu wana wawili, Manase na Efraimu.

21Wana wa Benyamini ni:

22Hawa ndio wana wa Raheli aliomzalia Yakobo; jumla yao ni kumi na wanne.

23Mwana wa Dani ni:

24Wana wa Naftali ni:

25Hawa walikuwa wana wa Bilha aliomzalia Yakobo, ambaye Labani alikuwa amempa Raheli binti yake; jumla yao walikuwa saba.

26Wote waliokwenda Misri pamoja na Yakobo, waliokuwa wazao wake hasa pasipo kuhesabu wakwe zake, walikuwa watu sitini na sita.

27Pamoja na wana wawili waliozaliwa na Yosefu huko Misri, jumla yote ya jamaa ya Yakobo, waliokwenda Misri, walikuwa sabini.

28Basi Yakobo akamtanguliza Yuda aende kwa Yosefu ili amwelekeze njia ya Gosheni. Walipofika nchi ya Gosheni,

29gari kubwa zuri la Yosefu liliandaliwa, naye akaenda Gosheni kumlaki baba yake Israeli. Mara Yosefu alipofika mbele yake, alimkumbatia baba yake, akalia kwa muda mrefu.

30Israeli akamwambia Yosefu, “Sasa niko tayari kufa, kwa kuwa nimejionea mwenyewe kwamba bado uko hai.”

31Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake na watu wa nyumbani mwa baba yake, “Nitapanda kwa Farao na kumwambia, ‘Ndugu zangu na watu wa nyumbani mwa baba yangu, waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, wamekuja kwangu.

32Watu hao ni wachunga mifugo, huchunga mifugo, wamekuja na makundi ya kondoo, mbuzi na ngʼombe pamoja na kila kitu walicho nacho.’

33Farao atakapowaita na kuwaulizeni, ‘Kazi yenu ni nini?’

34Mjibuni, ‘Watumwa wako wamekuwa wachunga mifugo tangu ujana wetu mpaka sasa, kama baba zetu walivyofanya.’ Ndipo mtakaporuhusiwa kukaa katika nchi ya Gosheni, kwa kuwa wachunga mifugo wote ni chukizo kwa Wamisri.”

← Mwanzo 45 Mwanzo Mwanzo 47 →