We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

Mwanzo 16

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← Mwanzo 15 Mwanzo Mwanzo 17 →

1Basi Sarai, mkewe Abramu, alikuwa hajamzalia watoto. Lakini alikuwa na mtumishi wa kike Mmisri jina lake Hagari,

2hivyo Sarai akamwambia Abramu, “Bwana amenizuilia kupata watoto. Nenda, ukakutane kimwili na mtumishi wangu wa kike, huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake.”

3Hivyo baada ya Abramu kuishi katika nchi ya Kanaani miaka kumi, Sarai akamchukua mtumishi wake wa kike wa Kimisri, Hagari na kumpa mumewe awe mke wake.

4Akakutana kimwili na Hagari, naye akapata mimba.

5Ndipo Sarai akamwambia Abramu, “Unawajibika na manyanyaso ninayoyapata. Nilimweka mtumishi wangu mikononi mwako, sasa kwa vile anajua kwamba ana mimba, ananidharau mimi. Bwana na aamue kati yako na mimi.”

6Abramu akamwambia, “Mtumishi wako yuko mikononi mwako. Mtendee lolote unalofikiri ni bora zaidi.” Ndipo Sarai akamtesa Hagari, hivyo akamtoroka.

7Malaika wa Bwana akamkuta Hagari karibu na chemchemi huko jangwani; ilikuwa chemchemi ile iliyokuwa kando ya barabara iendayo Shuri.

8Malaika akamwambia, “Hagari, mtumishi wa Sarai, umetokea wapi, na unakwenda wapi?”

9Ndipo malaika wa Bwana akamwambia, “Rudi kwa bibi yako ukajishushe chini yake.”

10Malaika akaendelea akasema, “Nitazidisha wazao wako, hivi kwamba watakuwa wengi mno wasiohesabika.”

11Pia malaika wa Bwana akamwambia:

12Atakuwa punda-mwitu katikati ya wanadamu,

13Hagari akampa Bwana aliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi,” kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.”

14Ndiyo sababu kisima kile kikaitwa Beer-Lahai-Roi,16:14 Beer-Lahai-Roi maana yake Yeye Aliye Hai Anionaye Mimi. ambacho bado kipo huko hata leo kati ya Kadeshi na Beredi.

15Hivyo Hagari akamzalia Abramu mwana, naye Abramu akamwita huyo mwana Hagari aliyemzalia, Ishmaeli.

16Abramu alikuwa na umri wa miaka themanini na sita wakati Hagari alipomzalia Ishmaeli.

← Mwanzo 15 Mwanzo Mwanzo 17 →