1Neno la Bwana likanijia kusema:
2“Mwanadamu, toa unabii na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
3Kwa kuwa siku ile imekaribia,
4Upanga utakuja dhidi ya Misri,
5Kushi30:5 Kushi ndiyo Ethiopia. na Putu, Ludi na Arabia yote, Libya30:5 Libya ndiyo Kubu. na watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri.
6“ ‘Hili ndilo Bwana asemalo:
7“ ‘Hizo nchi zitakua ukiwa
8Ndipo watakapojua kwamba mimi ndimi Bwana,
9“ ‘Siku hiyo wajumbe watatoka kwangu kwa merikebu, ili kuwatia hofu Ethiopia, wakiwa katika hali yao ya kuridhika. Maumivu makali yatawapata siku ya maangamizi ya Misri, kwa kuwa hakika itakuja.
10“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
11Yeye na jeshi lake, taifa lililo katili kuliko mataifa yote,
12Nitakausha vijito vya Naili
13“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
14Nitaifanya Pathrosi30:14 Pathrosi ni Misri ya Juu. kuwa ukiwa
15Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu,30:15 Kiebrania ni Sini.
16Nitaitia moto nchi ya Misri;
17Wanaume vijana wa Oni30:17 Yaani Heliopoli (Mji wa Jua). na wa Pi-Besethi30:17 Yaani Bubasti.
18Huko Tahpanhesi mchana utatiwa giza
19Kwa hiyo nitaipiga Misri kwa adhabu,
20Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa kwanza, siku ya saba, neno la Bwana likanijia kusema:
21“Mwanadamu, nimevunja mkono wa Farao mfalme wa Misri. Haukufungwa ili upone au kuwekewa kipande cha ubao ili upate nguvu za kuweza kuchukua upanga.
22Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume na Farao mfalme wa Misri. Nitavunja mikono yake yote miwili, ule mkono ulio mzima pia na ule uliovunjika na kuufanya upanga uanguke toka mkononi mwake.
23Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi zote.
24Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli na kuutia upanga wangu mkononi mwake, lakini nitavunja mikono ya Farao, naye atalia kwa huzuni mbele yake kama mtu aliyetiwa jeraha la kumfisha.
25Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli, lakini mikono ya Farao italegea. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana, nitakapoutia upanga wangu mkononi mwa mfalme wa Babeli, naye ataunyoosha dhidi ya Misri.
26Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi mbalimbali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.”