1Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,
2wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana):
3wazao wa Paroshi
4wazao wa Shefatia
5wazao wa Ara
6wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu)
7wazao wa Elamu
8wazao wa Zatu
9wazao wa Zakai
10wazao wa Bani
11wazao wa Bebai
12wazao wa Azgadi
13wazao wa Adonikamu
14wazao wa Bigwai
15wazao wa Adini
16wazao wa Ateri (kupitia Hezekia)
17wazao wa Besai
18wazao wa Yora
19wazao wa Hashumu
20wazao wa Gibari
21watu wa Bethlehemu
22watu wa Netofa
23watu wa Anathothi
24watu wa Azmawethi
25wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi
26wazao wa Rama na Geba
27watu wa Mikmashi
28watu wa Betheli na Ai
29wazao wa Nebo
30wazao wa Magbishi
31wazao wa Elamu ile ingine
32wazao wa Harimu
33wazao wa Lodi, Hadidi na Ono
34wazao wa Yeriko
35wazao wa Senaa
36Makuhani:
37wazao wa Imeri
38wazao wa Pashuri
39wazao wa Harimu
40Walawi:
41Waimbaji:
42Mabawabu wa lango la Hekalu:
43Watumishi wa Hekalu:2:43 Yaani Wanethini (pia 2:58, 70).
44wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni,
45wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu,
46wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani,
47wazao wa Gideli, Gahari, Reaya,
48wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu,
49wazao wa Uza, Pasea, Besai,
50wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu,
51wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
52wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
53wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
54wazao wa Nesia na Hatifa.
55Wazao wa watumishi wa Solomoni:
56wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
57wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami.
58Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni
59Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
60wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda
61Kutoka miongoni mwa makuhani:
62Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.
63Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.2:63 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.
64Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360;
65tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200.
66Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245,
67ngamia 435 na punda 6,720.
68Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake.
69Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,0002:69 Darkoni 61,000 za dhahabu ni sawa na kilo 500. za dhahabu, mane 5,0002:69 Mane 5,000 za fedha ni sawa na kilo 2,900. za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.
70Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.