We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

Mhubiri 9

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← Mhubiri 8 Mhubiri Mhubiri 10 →

1Kwa hiyo niliyatafakari yote haya nikafikia uamuzi kwamba waadilifu na wenye hekima na yale wanayoyafanya yako mikononi mwa Mungu, lakini hakuna mtu ajuaye kama anangojewa na upendo au chuki.

2Wote wanayo hatima inayofanana, mwadilifu na mwovu, mwema na mbaya, aliye safi na aliye najisi, wale wanaotoa dhabihu na wale wasiotoa.

3Huu ni ubaya ulio katika kila kitu kinachotendeka chini ya jua: Mwisho unaofanana huwapata wote. Zaidi ya hayo, mioyo ya watu, imejaa ubaya na kuna wazimu mioyoni mwao wangali hai, hatimaye huungana na waliokufa.

4Yeyote aliye miongoni mwa walio hai analo tumaini, hata mbwa hai ni bora kuliko simba aliyekufa!

5Kwa maana walio hai wanajua kwamba watakufa,

6Upendo wao, chuki yao na wivu wao

7Nenda, kula chakula chako kwa furaha, unywe divai yako kwa moyo wa shangwe, kwa maana sasa Mungu anakubali unachofanya.

8Daima uvae nguo nyeupe na daima upake kichwa chako mafuta.

9Furahia maisha na mke wako, umpendaye, siku zote za maisha ya ubatili uliyopewa na Mungu chini ya jua, siku zote za ubatili. Kwa maana hili ndilo fungu lako katika maisha na katika kazi yako ya taabu chini ya jua.

10Lolote mkono wako upatalo kufanya, fanya kwa nguvu zako zote, kwa kuwa huko kuzimu, unakokwenda, hakuna kufanya kazi wala mipango wala maarifa wala hekima.

11Nimeona kitu kingine tena chini ya jua:

12Zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ajuaye wakati saa yake itakapokuja:

13Pia niliona chini ya jua mfano huu wa hekima ambao ulinivutia sana:

14Palikuwa na mji mdogo uliokuwa na watu wachache ndani yake. Mfalme mwenye nguvu akainuka dhidi yake, akauzunguka akaweka jeshi kubwa dhidi yake.

15Katika mji huo kulikuwepo mtu mmoja maskini lakini mwenye hekima, naye akauokoa ule mji kwa hekima yake. Lakini hakuna aliyemkumbuka yule maskini.

16Kwa hiyo, nikasema, “Hekima ni bora kuliko nguvu.” Lakini hekima ya maskini imedharauliwa, wala hakuna anayesikiliza maneno yake.

17Maneno ya utulivu ya mwenye hekima

18Hekima ni bora kuliko silaha za vita,

← Mhubiri 8 Mhubiri Mhubiri 10 →