1Habari za ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Abrahamu:
2Abrahamu akamzaa Isaki,
3Yuda akawazaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari,
4Aramu akamzaa Aminadabu,
5Salmoni akamzaa Boazi, na mama yake Boazi alikuwa Rahabu,
6Yese akamzaa Daudi ambaye alikuwa mfalme.
7Solomoni akamzaa Rehoboamu,
8Asa akamzaa Yehoshafati,
9Uzia akamzaa Yothamu,
10Hezekia akamzaa Manase,
11wakati wa uhamisho wa Babeli, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake.
12Baada ya uhamisho wa Babeli:
13Zerubabeli akamzaa Abiudi,
14Azori akamzaa Sadoki,
15Eliudi akamzaa Eleazari,
16naye Yakobo akamzaa Yosefu ambaye alikuwa mumewe Maria, mama yake Yesu, aitwaye Kristo.1:16 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
17Hivyo, kulikuwepo na jumla ya vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli, na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli hadi Kristo.
18Basi Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria mama yake alikuwa ameposwa na Yosefu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Maria alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
19Kwa kuwa Yosefu, mwanaume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Maria hadharani, aliazimu kumwacha kwa siri.
20Lakini mara alipoazimu kufanya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto na kusema, “Yosefu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
21Naye atamzaa mwana, nawe utamwita Jina lake Yesu,1:21 Yesu ni Iesous kwa Kiyunani, na kwa Kiebrania ni Yoshua au Yeshua. Maana yake ni Yehova ni wokovu. kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.”
22Haya yote yalitukia ili litimie lile Bwana alilokuwa amenena kupitia nabii, akisema:
23“Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita Jina lake Imanueli”: maana yake, “Mungu pamoja nasi.”
24Yosefu alipoamka kutoka usingizini, akafanya kama vile alivyoagizwa na malaika wa Bwana, akamchukua Maria kuwa mke wake.
25Lakini hawakukutana kimwili mpaka Maria alipojifungua mwanawe kifungua mimba akamwita Jina lake Yesu.