We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

2 Nyakati 4

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← 2 Nyakati 3 2 Nyakati 2 Nyakati 5 →

1Mfalme Solomoni akatengeneza madhabahu ya shaba yenye urefu wa dhiraa ishirini,4:1 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9. upana wa dhiraa ishirini na kimo chake dhiraa kumi.4:1 Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5.

2Akatengeneza Bahari ya kusubu, yenye umbo la mviringo, ya dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo na kimo cha dhiraa tano. Kamba ya urefu wa dhiraa thelathini4:2 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5. ingeweza kuizunguka.

3Chini ya huo ukingo, kulikuwa na mafahali kuizunguka, yaani mafahali kumi katika kila dhiraa moja.4:3 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45. Hayo mafahali waliyasubu katika safu mbili yakiwa ya kitu kimoja na hiyo Bahari.

4Bahari hiyo ilikaa juu ya mafahali kumi na wawili, mafahali watatu walielekeza nyuso zao kaskazini, watatu magharibi, watatu kusini na watatu mashariki. Bahari hiyo ilikaa juu ya hao mafahali, nazo sehemu zao za nyuma zilielekeana.

5Unene wake ulikuwa nyanda nne,4:5 Nyanda nne ni sawa na sentimita 7.5. na ukingo wake ulifanana na ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi iliyochanua. Iliweza kuchukua bathi 3,000.4:5 Bathi 3,000 ni sawa na lita 60,000.

6Kisha akatengeneza masinia kumi kwa ajili ya kuoshea vifaa, naye akayaweka matano upande wa kusini na matano upande wa kaskazini. Ndani yake ndimo walioshea vifaa vya kutumika katika sadaka za kuteketezwa, lakini ile Bahari ilikuwa ni kwa ajili ya makuhani kunawia.

7Akatengeneza vinara vya taa kumi vya dhahabu kama ilivyoainishwa kwao na kuviweka hekaluni, vinara vitano upande wa kusini na vitano upande wa kaskazini.

8Akatengeneza meza kumi na kuziweka hekaluni, tano upande wa kusini na tano upande wa kaskazini. Pia akatengeneza mabakuli 100 ya dhahabu ya kunyunyizia.

9Akatengeneza ukumbi wa makuhani na ukumbi mwingine mkubwa na milango yake, naye akaifunika hiyo milango kwa shaba.

10Akaweka ile Bahari upande wa kusini, kwenye pembe ya kusini mashariki ya nyumba.

11Pia akatengeneza masufuria, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia.

12zile nguzo mbili;

13yale makomamanga 400 kwa ajili ya hizo nyavu mbili (safu mbili za makomamanga kwa kila wavu yakipamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo);

14vishikio pamoja na masinia yake;

15hiyo Bahari na hao mafahali kumi na wawili chini yake;

16pia hayo masufuria, masepetu, uma za nyama na vyombo vingine vyote vilivyohusiana.

17Mfalme aliagiza wavisubu vitu hivi kwenye kalibu za udongo wa mfinyanzi katika uwanda wa Yordani kati ya Sukothi na Sereda.4:17 Au Sarethani.

18Vitu hivi vyote Mfalme Solomoni alivyotengeneza vilikuwa vingi sana hivi kwamba uzito wa shaba haungekadirika.

19Solomoni pia akatengeneza samani zote zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mungu:

20vinara vya taa vya dhahabu safi pamoja na taa zake ili ziwake mbele ya sehemu takatifu ya ndani kama ilivyoelekezwa;

21maua ya dhahabu yaliyofanyizwa, taa na makoleo (vilikuwa vya dhahabu bora kabisa);

22mikasi ya dhahabu safi, mabakuli ya kunyunyizia, masinia na vyetezo; milango ya dhahabu ya Hekalu: yaani milango ya ndani ya Patakatifu pa Patakatifu, na milango ya ukumbi mkuu.

← 2 Nyakati 3 2 Nyakati 2 Nyakati 5 →