We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

2 Wakorintho 6

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← 2 Wakorintho 5 2 Wakorintho 2 Wakorintho 7 →

1Kama watendakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msipokee neema ya Mungu bure.

2Kwa maana asema:

3Hatuweki kitu cha kukwaza katika njia ya mtu yeyote, ili huduma yetu isionekane kuwa na lawama.

4Bali kama watumishi wa Mungu tuonyeshe kwa kila njia: katika saburi nyingi; katika dhiki, katika misiba, na katika shida;

5katika kupigwa, katika kufungwa gerezani na katika ghasia; katika kazi ngumu, katika kukesha na katika kufunga;

6katika utakatifu, katika ufahamu, katika uvumilivu, na katika utu wema; katika Roho Mtakatifu na upendo wa kweli;

7katika maneno ya kweli na katika nguvu za Mungu, kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;

8katika utukufu na katika kudharauliwa; katika sifa mbaya na katika sifa nzuri; tukiwa kama wadanganyaji, lakini tukiwa wakweli;

9tukiwa maarufu, lakini tukihesabiwa kama tusiojulikana; tukiwa kama wanaokufa, lakini tunaishi; tukipigwa, lakini hatuuawi;

10tukiwa kama wenye huzuni, lakini siku zote tukifurahi; tukionekana maskini, lakini tukitajirisha wengi; tukiwa kama wasio na kitu, lakini tuna vitu vyote.

11Tumesema nanyi wazi, enyi Wakorintho na kuwafungulieni mioyo yetu wazi kabisa.

12Sisi hatujizuii kuwapenda, bali ninyi mmeuzuia upendo wenu kwetu.

13Sasa nasema, kama na watoto wangu: Ninyi pia ifungueni mioyo yenu kabisa.

14Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza?

15Kuna mapatano gani kati ya Kristo na Beliari?6:15 Beliari hapa ina maana ya uovu, kutokumcha Mungu. Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini?

16Kuna mapatano gani kati ya Hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema: “Nitakaa pamoja nao na kutembea katikati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”

17“Kwa hiyo tokeni miongoni mwao,

18“Mimi nitakuwa Baba kwenu,

← 2 Wakorintho 5 2 Wakorintho 2 Wakorintho 7 →