We Believe JesusFé, Esperança e Nova Vida

1 Nyakati 24

Biblica® Toleo Wazi la Neno: Biblia Takatifu™ · suaíli

← 1 Nyakati 23 1 Nyakati 1 Nyakati 25 →

1Hii ndiyo migawanyo ya wana wa Aroni:

2Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakahudumu kama makuhani.

3Akisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Aroni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao.

4Idadi kubwa ya viongozi walipatikana miongoni mwa wazao wa Eleazari, kuliko miongoni mwa wazao wa Ithamari, nao waligawanywa kwa uwiano: Viongozi kumi na sita kutoka jamaa ya wazao wa Eleazari na viongozi wanane kutoka jamaa ya wazao wa Ithamari.

5Waliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari.

6Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.

7Kura ya kwanza ilimwangukia Yehoyaribu,

8ya tatu Harimu,

9ya tano Malkiya,

10ya saba Hakosi,

11ya tisa Yeshua,

12ya kumi na moja Eliashibu,

13ya kumi na tatu Hupa,

14ya kumi na tano Bilga,

15ya kumi na saba Heziri,

16ya kumi na tisa Pethahia,

17ya ishirini na moja Yakini,

18ya ishirini na tatu Delaya,

19Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la Bwana kulingana na masharti waliyoelekezwa na Aroni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.

20Kuhusu wazao wa Lawi waliobaki:

21Kwa wa Rehabia, kutoka kwa wanawe:

22Kutoka kwa Waishari: alikuwa Shelomithi,

23Wana wa Hebroni: Yeria alikuwa mkuu, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.

24Mwana wa Uzieli: alikuwa Mika;

25Ndugu yake Mika: alikuwa Ishia;

26Wana wa Merari: walikuwa Mahli na Mushi.

27Wana wa Merari:

28Kutoka kwa Mahli: alikuwa Eleazari, ambaye hakuwa na wana.

29Kutoka kwa Kishi: mwana wa Kishi:

30Nao wana wa Mushi: walikuwa Mahli, Ederi na Yeremothi.

31Pia walipiga kura kama vile ndugu zao wazao wa Aroni walivyofanya, mbele ya Mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na mbele ya viongozi wa jamaa ya makuhani na ya Walawi. Jamaa za ndugu wakubwa zilitendewa sawasawa na zile za ndugu wadogo.

← 1 Nyakati 23 1 Nyakati 1 Nyakati 25 →